Watu sita wafariki dunia kwa ajali ya barabarani Dodoma

Watu sita wafariki dunia kwa ajali ya barabarani Dodoma

By


Watu sita wamefariki dunia papo hapo huku wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mkoani Dodoma.
Eneo la ajali ambapo watu sita wamefariki baada
Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gillece Muroto amesema ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 4, 2018 majira ya mchana ambapo daladala aina ya Toyota Hiace iliyokuwa na abiria kugongana na lori la kubebea taka.
Taarifa zaidi nitazitoa baada ya kufuatilia lakini kwa ufupi ajali hiyo ipo na watu sita wamekufa na wengine sita wapo katika hospitali ya rufaa ya mkoa na hali zao sio nzuri,” amesema Muroto kwenye mahohjiano na Gazeti la Mwananchi.

Comments