TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAR 04.03.2018
Riyad Mahrez
Arsenal inatarajiwa kujiunga katika kuwania kumsajili mchezaji wa kiungo
cha kati wa Leicester Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 26. (Daily
Star Sunday)
Meneja wa Leicester Claude Puel anasaema "hamfikrii" Mahrez, ambaye
hajaonekana katika kalbu hiyo tangu pendekezo la uhamisho wake kwenda
Manchester City litibuke kufuatia kuwadia kwa muda wa mwisho wa
uhamisho. (Mail on Sunday)
Muungano wa wachezaji soka kitaaluma umejitolea kusaidia kutatua hali
baina ya mchezaji raia wa Algeria Mahrez na timu ya Leicester City. (Sun
on Sunday)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafikiria kumlipia Maurizio Sarri
Euro milioni 8 katika mkataba wake ili aweze kumsajili kocha huyo wa
Napoli kuwa meneja mpya wa timu yake.(La Gazzetta dello Sport - in
Italian)Conte aliteuliwa kuifunza Chelsea baada ya kuisimamia timu ya Italia katika michuano ya Euro mnamo 2016
Huenda bosi wa Chelsea Antonio Conte akafutwa kazi iwapo upande wake utashindwa na Watford Jumatatu. (Sunday Express)
Conte ameiambia Chelsea kuwa wanaihitaji kuwasajili wachezaji wawili au
watatu wa kiwango cha kimataifa kuweze kulinyanyua taji la ligi msimu
ujao, na ametaja kuwasili kwa wachezaji wengi kama mojawapo ya kushindwa
kwao kulilinda taji lao msimu huu. (Sunday Telegraph)
Kipa wa Manchester City mwenye umri wa miaka 30, Joe Hart,
aliyechukuliwa kwa mkopo huko West Ham, atalengwa na Chelsea iwapo
Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 25 ataondoka katika klabu hiyo
msimu huu wa joto. (Sun on Sunday)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Ross Barkley, huedna amepata
jereha la msuli wa paja ambalo iwapo litathibitishwa , litamfanya
mchezaji huyo raia wa England kuwa mchezaji wa nane katika klabu hiyo
kukabiliwna tatizo hilo msimu huu. (Sunday Telegraph)
Manchester United wapo katika hatua kubwa ya mazungumzo ya kumchukua
winga wa Ajax mwenye umri wa miaka 18 Justin Kluivert msimu huu wa joto -
ambaye ni mwanawe mchezaji wa zamani wa Barcelona Patrick. (Sunday
Mirror)Mesut Ozil na Rihanna
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil ametangaza kuwa
Rihanna ndio "bahati yake" baada ya muimbaji huyo kutazama ushindi wa
Arsenal dhidi ya Everton. Rihanna pia alisherehekea na Ozil na wachezaji
wenziwe ushindi wa Ujerumani katika kombe la dunia mnamo 2014 nchini
Brazil. (London Evening Standard)
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, yupo tayari kuingia Real Madrid
lakini mchezaji mwenzake wa timu ya kimataifa Dele Alli, mwenye umri wa
miaka 21, hayuko tayari kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Liverpool
kiungo cha kati, Graeme Souness. (Sunday Times )
Real Madrid ipo tayari kuongeza mshahara wa Cristiano Ronaldo hadi Euro
milioni 30 kwa mwaka kuanzia msimu huu wa joto, na kumfanya mchezaji
huyo mwenye umri wamiaka 32 raia wa Ureno kuwa juu pamoja na mwenzake
Neymar ki malipo ya mwaka. (ABC, via Marca)
Edin Dzeko aliipuza Chelsea ili asalie Roma kwasababu ya maisha yake
'yasio halisi' Italia, licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 31 raia wa Bosnia na Herzegovina anasema ni 'heshima kubwa' kwamba
The Blues' inamtaka. (Klix, via Mail on Sunday)
Everton imempa ruhusa aliyekuwa kaimu mkuu wa zamani David Unsworth,
ruhusa kuzungumza na Oxford United kuhusu pengo lao la kazi ya
usimamizi. (Sky Sports)
Jose Mourinho
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameshutumu kwa mara nyingine
hisia iliopo Old Trafford, and claims the noise made at Portsmouth's
Fratton Park is better. (London Evening Standard)
Mourinho amelenga kumsajili mchezajiwa kiungo cha kati wa Bayern Munich
raia wa Chile Arturo Vidal, mwenye umri wa miaka 30, katika msimu ujao
wa joto huku kukiwepo wasiwasi kuhusu ukosefu wa nafasi zaidi katika
kiungo hicho. (Manchester Evening News)
Mkuu wa West Brom Alan Pardew anawataka maafisa wa Baggies wamshawishi
Jonny Evans akubali makubaliano mapya ya kumhifadhi mlinzi huyo mwenye
umri wa miaka 30 kutoka Ireland ya kaskazini dhidi ya timu nyingine za
Ligi ya England. (Birmingham Mail)Bakary Sako
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace raia wa Mali Bakary Sako,
mwenye umri wamiaka 29, ameondolewa kwa siku zilizosalia msimu huu
kutokanana kuumiza mishipa na jicho la mguu. Ametuma ujumbe wa matumaini
katika mtandao wa kijamii.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anasisitiza kuwa mshambuliaji Sadio Mane
hana wivu na mshambuliaji mwenza Mohamed Salah na kwamba wachezaji hao
raia wa Senegal na Misri ni 'marafiki wa dhati'. (Sunday Mirror)
Klopp anasema hana shinikizo kutoka kwa wamiliki wa Liverpool kwasbabau
hawasemi, "mwaka ujao muwe mabingwa la sivyo unaweza kuondoka" na badala
yake " ni watu wanje wanaosema , asipoleta taji, yupo kwenye
shinikizo'." (Mail on Sunday)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Didi Hamann anaamini
klabu hiyo badu ina mapungufu katika upande wa ulinzi , licha ya
kumsajili bekiwa kati raia wa Uholanzi Virgil van Dijk, kwa thamani ya
pauni milioni 75 mapema mwezi Januari. (Omnisport, via Liverpool Echo)
Share:
Comments
Post a Comment