HABARI
Masheikh watano waliokamatwa na watu wasiojuliakana waachiwa huru
Mashehe watano waliotoweka kuanzia Febuari 9 mwaka huu huko Zanzibar wameachiwa katika mazingira ya kutatanisha na kurejea katika familia zao usiku wa kuamkia Machi 4, 2018.“Mimi na wenzangu wanne tulipelekwa kusikojulikana na baada ya kuhojiwa wametuachia tukiwa salama,” mmoja wa mashehe hao, Amir Haji Khamis Haji aliiambia Azam Tv.
“Wale waliotukamata hawakuwa na nia mbaya…walikuwa wakitekeleza kazi yao ya usalama…na ndio maana baada tu ya kugundua kwamba sihusiki na y ale waliyokuwa wakinihoji waliniachia huru na nimerudi nyumbani…niko na familia yangu,” alisema Khamis.
Hudhuni ya muda mrefu ya wanafamilia wa Shehe Khamis iliyeyuka mara baada ya ndugu yao kurejea nyumbani akiwa salama.
“Tulikuwa na hofu kwamba yawezekana ametupwa baharini au vinginevyo, lakini tunamshukuru sana Mungu kwa kumrejesha akiwa salama,” alisema mke wa Shehe Khamis, Mwanaunguja Hadhar baada ya mumewe kurejea nyumbani.
Comments
Post a Comment